About St. Theresia Parish

Mt. Theresia wa Mtoto Yesu
KUZALIWA
Mt. Teresia wa Mtoto Yesu anayejulikana kama Ua dogo la Upendo alizaliwa tarehe 2 Januari 1873 Alençon, Ufaransa. Baba yake aliitwa Louis Martin ambaye alikuwa fundi saa na sonara, na mama yake aliitwa Zélie Guérin ambaye naye alikuwa mtengeneza lesi. Baba yake alitaka kuwa mmonaki na mama yake alitaka kuwa mtakatifu. Wote wawili walitaka kuishi maisha ya kutohusiana kimwili. Lakini Padre mmoja aliwashauri maana ya ndoa na mpango wa Mungu wa ndoa. Katika familia yake walizaliwa wakiwa watoto tisa. Watoto wanne walifariki dunia bado wakiwa wadogo, wavulana wawili na wasichana wawili. Wasichana wote watano (Marie, Pauline, Leonie, Celine na Theresia) walikuwa watawa katika shirika la Karmeli. Theresia alikuwa mtoto wa mwisho na jina lake lilikuwa Francoise-Marie Therese. Akiwa mtoto aliishi kwa furaha.
ELIMU YAKE
Theresia alipata elimu yake katika konventi ya wabenediktini wa Notre- Dame-du-Pre. (Mama yetu wa Pre). Lakini hakuwa na furaha. Mwaka 1886 aliacha shule akaanza kusoma masomo binafsi.
KUPONYWA NA KUPOKEA KOMUNIO YA KWANZA
Mwishoni mwa mwaka 1882 Mt. Theresia alianza kupata kizunguzungu cha mara kwa mara. Mwaka wa 1883 akapatwa na ugonjwa wa ajabu. Akawa anamwomba Bikira Maria wa Malkia wa Mbingu, alimwomba amhurumie na kumwondolea maumivu. Siku ya sherehe ya Pentekoste mwaka 1883 aliponywa ugonjwa wake baada ya kuona sanamu ya Bikira Maria iliyokuwa chumbani mwake ikitabasamu. Baada ya hapo akarudi shule kuendela na masomo. Alifundishwa na wamonaki wa kibenediktini wa Lisieux na baada maandalizi ya kina yaliyofikia kilele chake katika uzoefu wa wazi wa kuwa karibu sana na Kristo, akapataKomunio ya kwanza tarehe 8 Mei 1884. Alipata Sakramenti ya kipaimara tarehe 14 juni mwaka huo huo wa 1884.
HAMU YAKE YA KUWA MTAWA
Theresia naye akiwa na miaka tisa alitamani naye kuingia katika maisha ya utawa. Baadaye hata dada yake Marie naye alijiunga na maisha ya utawa. Kitendo hicho kilizidisha hamu ya Theresia ya kutaka kuwa mtawa. Akiwa na umri wa miaka 14 aliamua kuwa hata yeye anataka kuwa mtawa katika konventi ya Karmeli Lisieux. Lakini askofu alikataa akasema asubiri mpaka atimize miaka 21.
SABABU ZA KUITWA THERESIA WA MTOTO YESU
Wakati wa kesha la Noeli siku chache kabla ya kufikisha miaka 14, alipata hali fulani ambayo yeye anaiita kuongoka kwake. Maisha yake ya ndani yalipata nguvu za ajabu. Baada ya hali hiyo alisema kuwa Usiku ule Mtoto Mtakatifu alikuwa amemponyahisia zake kali na kumviringishia silaha zake. Hii ndio maana anaitwa Theresia wa Mtoto Yesu. Mwaka uliofuata akamwambia baba yake kuwa anataka kuwa mkarmeli.
THERESIA ANAKATALIWA KUINGIA UTAWA AKIWA MDOGO
Mt. Theresia alimwambia baba yake kuwa anataka kuwa mkarmeli. Baba yake alikubali lakini Viongozi wa shirika na askofu Hugonin wa Bayeux walikataa kwa sababu ya umri wake. Theresia alitamani suala hilo lifike kwa Papa. Alipata nafasi ya kumtembelea Papa Leo XIII ikiwa ni sehemu ya hija yao Roma. Alipopata nafasi ya kupita mbele ya Papa alitaka kumwomba Papa ruhusa ili aingie karmeli akiwa na miaka 15 lakini Mons. Reverony alimuwahi na kumwambia Papa kuwa anataka kuingia utawa akiwa mdogo na Papa akamwambia kuwa Mungu akipenda atakuwa mtawa. Kitendo hicho kilimuumiza sana kiasi kwamba alikiita kishawishi ambacho ilibidi apate nguvu kutoka kwa Mungu ili aweze kuyavumilia hayo yote.
KUINGIA KARMELI YA LISIEUX
Mt. Theresia aliingia Karmeli ya Lisieux tarehe 9 Aprili mwaka 1888. Alipokea vazi tarehe 10 Januari mwaka 1889, na akaweka nadhiri zake Septemba 8, 1890 katika sherehe ya kuzaliwa kwa Bikira Maria. Imani yake ilijaribiwa kwa kifo cha baba yake kilichotokea tarehe 29 Julai mwaka 1894. Hata hivyo Theresia alikuwa katika utakatifu, akiongozwa na mwanga wa Neno la Mungu na aliongozwa na Injili akiuweka upendo katikati ya kila kitu.
HAMU YAKE NA WITO WAKE
Theresia alitamani sana kuwa mtume tangu mwanzo kabisa mwa maisha yake. Alitamani sana kuokoa roho za watu wengi wakiwemo mapadre. Ili kutimiza azima yake hiyo alitamani sana kutekeleza miito mbalimbali.Alitamani awe mhubiri, mtume, mmishonari, na shahidi. Hata hivyo ilikuwa tu baada ya yeye kujitoamwenyewe akimiminwa katika Mungu na alijikabidhi mwenyewe kwa huruma Upendo ndipo alipogundua wito ambao Mungu alimwitia. Alisema hivi “Nimeelewa kwamba upendo hushikilia miito yote.Natambua kwamba tamaa zangu zote zimetimilika. Nimepata wito wangu. Katika moyo wa Kanisa, mama yangu, mimi nitakuwa upendo.”
MAFUNDISHO YAKE - NJIA NDOGO YA UTOTO
Mafundisho yake yanafahamika kama “njia ndogo”. Alijawa na upendo wa Mungu na akajitoa kabisa kwa upendo huo. Alijua jinsi ya kuuweka katika vitendo kwa majirani zake katika njia ya kawaida kabisa. Hamu yake kubwa ilikuwa kumwona kila mtu akiangazwa na mwanga wa imani. Katika kutafuta jinsi ya kuitekeleza hiyo sauti ndipo alipogundua kuwa “wito wake alikuwa awe upendo katika moyo wa Kanisa“. Ndipo hapo alipotembea katika njia ndogo ya watoto ya kujiachilia mikononi mwa Mungu. Ujumbe wake mkuu ni kuwa na tabia ya kitoto mbele ya Mungu. Aliona neema ya Kristo katika maisha yake. Mt. Theresia anawaita watu kuwa na ukarimu usio na ukomo na kuwakaribisha katika moyo wa Kanisa kuwa mitume na mashahidiwakereketwa wa upendo wa Kristo.
THERESIA WA MTOTO YESU NA MAANDIKO MATAKATIFU
Teresia wa Mtoto Yesu hakuwa msomi lakini aliandika mambo ya msingi sana na ya kawaida yanayogusa maisha ya watu wengi. Wakati anaandika kurasa zake juu ya Maandiko Matakatifu, ilikuwa kabla ya Mtaguso wa Pili wa Vatican uliosisitiza umuhimu wa Maandiko Matakatifu katika maisha ya wakristo. Aliandika yale ambayo baadae yalikuja kusisitizwa na Mtaguso wa Pili wa Vatican. Aliwahi kuandika hivi:
“Ndiyo, inaonekana kwangu kuwa sikuwahi kutafuta kitu kingine zaidi ya ukweli”.
Ukweli ambao alikuja kuupata katika Injili. Aligundua kuwa Maandiko Matakatifu ni muhimu kwani yanatufunulia Neno wa Mungu aliyefanyika mwili. Ndiyo maana alisema:
“Sipati tena kitu chochote katika vitabu isipokuwa katika Injili. Injili zinatosha”. Andika tena hivi
“Nioneshe siri zilizofichika kwenye Injili, Ah! kitabu cha dhahabu/mpenzi hazina yangu”. Alieleza huruma ya Mungu na haki yake.
KAZI YAKE
Kazi yake ilichapishwa baada ya kifo chake anajulikana kama “Historia ya roho” ambayo anaieleza kama njia ndogo.
KIFO CHAKE
Mt. Theresia alifariki dunia tarehe 30 mwezi wa tisa mwaka 1897 kwa ugongwa wa kifua kikuu. Alifariki akiwa na umri wa miaka 24 tu.
KUTANGAZWA MTAKATIFU NA MSIMAMIZI WA MISHENI
Alitangazwa mtakatifu na Papa Pius XI tarehe 17 Mei 1925. Papa huyo huyo akamtangaza kuwa mlinzi wa misheni zote duniani tarehe 14 Desemba 1927.
KUTANGAZWA MWALIMU WA KANISA
Mt. Theresia wa Lisieux, alitangazwa Mwalimu wa Kanisa na Papa Yohane Paul II Oktoba 19, 1997.

Our Parish History
UNUNUZI WA KIWANJA NA UJENZI WA KANISA LA MUDA
Asili ya Parokia ya Theresia wa Mtoto Yesu ni Parokia ya Mt. Peter Claver na Theresia wa Mtoto Yesu ya Mbezi Luis. (Parokia hii ilikuwa inasimamiwa na watakatifu wawili). Eneo hili lilinunuliwa na Parokia hii mwaka 2002/3. Awali lilikuwa ni shamba lililomilikiwa na muumini mmoja aliyeitwa Bwana Kaduri ambaye alipenda kuliuza kwa kanisa. Gharama za kukunua shamba hili ilitokana kwa kiasi kikubwa na michango ya waamini. Parokia ya Mt. Peter Claver/Theresia wa Mtoto Yesu ililinunua kwa lengo la kuhamishia Parokia eneo hilo kwa vile eneo kubwa la Parokia ya Mbezi Luis likiwemo kanisa lenyewe na nyumba ya mapadri lilikuwa kwenye eneo la hifadhi ya Barabara.
Mwaka 2005 uongozi wa Parokia chini ya Paroko Padri Peter, uliagiza waamini wanaozunguka eneo hili kwenye kiwanja wajenge kanisa la muda ili wapate mahali pa kusalia wakati Parokia ikijiandaa Kujenga kanisa jipya kubwa na la kisasa kwa ajili ya Parokia. Katika eneo hili kulikuwa na jumuiya tona ambazo ni Kibanda cha Mkaa, Mt. Fransinco wa Asis, Mt. Benedict, Mt. Fransisco Xavery na Mt. Scolastica. Jumuiya hizi zilijipanga kwa ajili ya kuanza kujenga kanisa la muda. Mwaka huo 2005 ilifanyika sherehe ya kipaimara katika viwanja hivi na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dara es Salaam ambaye alitoa kipaimara alibariki pia eneo hili na kuzindua ujenzi wa kanisa dogo ambao ulisimamiwa na viongozi wa Jumuiya zilizotajwa ambao waliunda kamati ya ujenzi mwenyekiti wake akiwa Ndugu Augustino Moshi na mweka hazina akiwa Mama Theodora Massawe.
Mwaka huo huo 2005 Parokia ya Mt. Peter Claver walipata eneo lilingine lililopakana na eneo la kanisa na kulinunua kwa ajili ya kujenga kanisa jipya pamoja na nyumba ya mapadri, hivyo wazo la kuhamia kwenye eneo lile jipya lilifutwa na wazo la kujenga kanisa eneo hilo pia lilifutwa. Hivyo kanisa lililokuwa linajengwa na jumuiya lililofikiriwa kuwa la muda ilibidi kuongezwa ukubwa ili kukidhi mahitaji ya waamini wa eneo hili ambao walikuwa wakiongezeka kwa kasi kubwa. Ilichukua mwaka mmoja kukamilisha kanisa hilo na mwaka 2006 Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, alipokuja tena kutoa kipaimara alitembelea kanisa na kufurahishwa na kazi iliyofanywa na kushauri ijengwe nyumba ya Mapadri.
KUTANGAZWA KUWA KIGANGO CHA MT. THERESIA WA MTOTO YESU
Baada ya kukamilika kanisa kwa kiasi cha kuridhisha, Mwaka 2006 mwezi September, uongozi wa Parokia chini ya Paroko Padri Vivian Menezes ulitangaza kuanzishwa Kigango cha Mt. Theresia wa Mtoto Yesu. Hivyo Mtakatifu Peter Claver alibaki kuwa msimamizi wa Parokia na Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu akahamishwa kuwa msimamizi wa Kigango. Taratibu nyingine za kuchagua viongozi wa kamati tendaji wa Kigango ulifanyika. Jumuiya pia zilianza kuongezeka kutoka jumuiya 5 hadi Jumuiya 15 na kanda 3. na pia kuweka mipaka upya kati ya kigango cha mt. Theresia wa Mtoto yesu na kile cha Mt. Maria Consolata- Makabe.
UZINDUZI WA PAROKIA
Agizo au pendekezo la Baba Kardinali la kujenga nyumba ya mapadri, liliwahamasisha waamini kwani lilionyesha dhahiri kwamba alikuwa na nia ya kuanzisha parokia mpya hapa. Hivyo waamini wa kigango walitafakari kwa makini juu ya hili na kuweka nia ya kuwa na nyumba ya mapadri. Hata hivyo haikuwa rahisi kuanza kujenga nyumba haraka haraka kwa sababu mbili, kwanza ni hali ya kuichumi na waamini wakati huo walikuwa wachache na ujenzi ungekuwa na gharama kubwa sana, na pili eneo lilikuwa halijapimwa na kupangiliwa kitu gani kikae wapi. Hivyo viongozi wa halmashauri walei kigango walipendekeza kufanya mazungumzo na muamini mmoja aliyekuwa na nyumba yake jirani na kanisa ambayo ilikuwa haikaliwi na mtu ili aitoe kwa kanisa kuwa nyumba ya mapadri kwa muda. Paroko aliafiki na kwa busara zake alifikisha pendekezo hilo kwa Kadinali ambaye aliridhia na kutoa kibali.
Baada ya Kadinali kuonyesha kukubali mazungumzo yalifanyika, na yule mwenye nyumba ile ambaye aliishi Zanzibar, aliitoa itumiwe na mapadri bure kwa muda wa miaka saba wakati tukiendelea kujenga nyumba yetu wenyewe. Ukarabati uliohitajika ulifanyika na nyumba iliweza kuwa na mazingira mazuri ya kuishi mapadri.
Tarehe 7 Oktoba mwaka 2007 Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam alizindua rasmi Parokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu na kuikabidhi kwa Shirika la Wakarmeli kuiendesha, na kumtangaza Padri Marlon Rodrigues kuwa Paroko wake wa kwanza na Padri Ivan Monteiro kuwa Paroko msaidizi
VIGANGO
Parokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu Mbezi Mwisho ilipoanza ilikabidhiwa vigango viwili ambavyo ni Kigango cha Mt. Maria Consolata Makabe na kigango cha Mt. Maria Benedikta wa Msalaba Msumi. Baada ya takriban mwaka mmoja kigango cha Makabe kilipandishwa hadhi na kuwa Parokia na kukichukua kigango cha Msumi, hivyo Parokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu ikabaki bila kuwa na kigango hadi mwaka 2010 wakati Padri Shabas Crasta akiwa Paroko, Parokia ilipokabidhiwa kigango cha Bikira Maria Imakulata Matosa ambacho awali kilikuwa chini ya Parokia ya Mbezi Beach ya Bikira Maria Mama wa Huruma. Baadaye mwaka 2014 wakati wa Paroko Padri Renatus Payovera, kilianzaishwa kigango cha Mt. Simon Stoki. Hivyo Parokia kuwa na vigango viwili.
Mwaka 2020 Baba Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dsm Yuda Thadei Rua’ichi alikipatia kigango cha Bikira Maria Immakulata hadhi ya kuwa Parokia Teule hivyo Parokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu Kubakia na kigango kimoja tu Cha Mt. Simon stock hadi havi leo.
IDADI YA WAAMINI
Parokia ina jumla ya kanda 22 na jumuiya 83 (Parokiani kanda 14, na jumuiya 57 Kigango cha Mt. Simon Stoki kanda 8 na jumuiya 26.), hii ikiwa ni wastani wa jumuiya 4 kwa kila kanda na kila jumuiya ina wastani wa familia au kaya 10 hadi 20. Kulingana na sensa ya parokia ya mwaka 2018 iliyofanyika kupitia jumuiya ndogondogo za kikristu, Parokia ina waamini wapatao 5460. Kati yao 1465 ni watoto na 3995 ni watu wazima

Our Mission
Kujenga Imani dhabiti na Madhubuti kwa Waamini
Our Current Leaders

Fr. Vivian Menezes, OCD
Parish Priest
Fr. Stanislaus Rodrigues, OCD
Assistant Parish Priest